MCHEZAJI wa zamani wa Manchester United, Gary Neville amedai kuwa kutojiamini kwa Manchester City ndio chanzo kikubwa cha matokeo mabovu yanayofifisha matumaini yao ya kutetea taji lao la Ligi Kuu. City wamejikuta wakiteleza mpaka nafasi ya nne katika msimamo wa ligi baada ya kujikuta wakipokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka Crystal Palace jana, kikiwa kipigo chao cha saba katika mechi 13 zilizopita walizocheza. City wanaonolewa na Manuel Pellegrini sasa wako nyuma ya vinara Chelsea kwa alama tisa huku wakiwa wamecheza mchezo mmoja zaidi na Neville hategemei tena kama wanaweza kurejea katika nafasi yao. Neville amesema tatizo kubwa linalowasumbua City ni kutojiamini ingawa wana kikosi imara chenye wachezaji wenye ubora wa hali ya juu. Beki huyo wa zamani wa United aliendelea kudai kuwa kwasasa hadhani kama City wataweza tena kuifikia Chelsea kwani mechi zilizobakia ni chache mno.
No comments:
Post a Comment