MSHAMBULIAJI mkongwe wa Chelsea, Didier Drogba amesisitiza jana kuwa anataka kucheza msimu mmoja zaidi kabla ya kuamua mustakabali wake. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 37 anatarajia kumaliza mkataba wake na vinara hao wa Ligi Kuu mwishoni mwa msimu huu toka kurejea Stamford Bridge baada ya kuondoka kwa misimu miwili. Akiulizwa kuhusu mustakabali wake Drogba amesema amafikiria sana suala hilo na ameamua kucheza msimu zaidi. Meneja wa Cheslea Jose Mourinho alikaririwa wiki iliyopita akidai kuwa bado hajazungumza na Drogba kuhusiana na mustakabali wake wa baadae. Mourinho alimsajili Drogba mara ya kwanza alipokuja kuinoa Chelsea mwaka 2004 akitokea Marseille ambapo mshambuliaji huyo alikuja kufunga mabao 157 katika msimu nane aliyokaa katika timu hiyo ikiwemo penati iliyowapa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment