Tuesday, April 14, 2015

PENATI ZAMKARAHISHA MESSI.

MSHAMBUIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amekiri kukerwa na jinsi alivyokosa penati nyingi msimu huu. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina ameshakosa penati nne kwa klabu na nchi yake mwaka huu ikiwemo ile ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City, Kombe la Mfalme dhidi ya Atletico Madrid na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Brazil. Messi mwenye umri wa miaka 27 amesema ingawa bado ndio mpiga penati wa Barcelona lakini anahisi inabidi aimarishe zaidi rekodi yake. Messi aliendelea kudai kuwa anadhabu magolikipa wameshagundua mbinu zake hivyo inabidi abadilishe ili washindwe kuzuia michomo yake wakati anapopiga.

No comments:

Post a Comment