Monday, April 20, 2015

EVRA ADAI FERGUSON ALIMTABIRIA KUJA KUWA KOCHA BORA.

BEKI wa kimataifa wa Ufaransa, Patrice Evra amebainisha mipango yake ya kuja kuwa kocha wakati atakapostaafu baada ya kudokezwa na meneja wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson. Beki huyo wa klabu ya Juventus, amecheza misimu saba akiwa chini Ferguson katika timu ya United kabla ya kocha huyo raia wa Scotland hajastaafu mwaka 2013. Hata hivyo, Ferguson ambaye amekuwa akiinoa United kwa miaka 26 hakuondoka Old Trafford bila kutoa ushauri kwa Evra kuhusu mustakabali wake wa mbeleni. Evra amesema kabla ya Ferguson hajaondoka alimuita ofisini kwake na kumwambia kuwa ana jambo anataka kumwambia. Beki huyo aliendelea kudai kuwa Ferguson alimwambia United kuna wachezaji wawili ambao wataweza kuja kuwa makocha bora kabisa na mmoja wapo ni yeye pamoja na Ryan Giggs. Kwasasa tayari Giggs ameshaanza kazi ya ukocha akiwa kama msaidizi wa Louis van Gaal katika kikosi cha United.

No comments:

Post a Comment