WAKALA wa mshambuliaji Radamel Falcao ameripotiwa kufanya mazungumzo na klabu ya Liverpool kwa ajili ya uwezekano wa nyota huyo kwenda Anfield akitokea AS Monaco. Mshambuliaji huyo kwasasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Manchester United lakini ameshindwa kung’aa baada ya kufunga mabao manne katika mechi 23 alizocheza. Meneja wa United Louis van Gaal ana uwezo wa kumbakisha Falcao moja kwa moja lakini taarifa kutoka nchini Hispania zinadai kuwa Mholanzi huyo amewaarifu Monaco kuwa watamrudisha nyota huyo wa kimataifa wa Colombia mwishoni mwa msimu huu. Falcao amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Chelsea na Liverpool hivi karibuni na wakala wake Jorge Mendes amesema amefanya mawasiliano na klabu kadhaa kwa ajili ya kumtafutia mahali papya nyota huyo wa zamani wa FC Porto na Atletico Madrid. Huku kukiwa na tetesi za kuondoka kwa washambuliaji Mario Balotelli, Rickie Lamberty na Fabio Borin katika timu ya Liverpool, Mendes anaripotiwa kutumia mwanya huo kumshawishi Brendan Rodgers kumsajili Falcao kwa mkataba wa moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment