MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Paris Saint-Germain amefungiwa kucheza mechi nne kwa kutoa lugha ya kuitusi Ufaransa wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ambao walifungwa na Bordeaux. Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden alinaswa katika picha za video akimtukana mwamuzi Lionel Jaffredo baada ya kipigo cha mabao 3-2 huku akidai nchi hiyo haikustahili kuwa na mchezaji mwenye kipaji kama yeye. Kauli hiyo ilizusha hasira kali miongoni mwa wananachi wa taifa hilo huku Waziri Mkuu wan chi hiyo naye alilaani vikali kauli ya Ibrahimovic. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 baadae aliomba radhi kwa kauli yake hiyo na kudai kuwa asingeweza kusaini kuichezea PSG kama angekuwa haipendi Ufaransa. Adhabu hiyo inamaanisha Ibrahimovic atakosa michezo ya ligi ambayo PSG itacheza dhidi ya Nice, Lille, Metz na Nantes.
No comments:
Post a Comment