Sunday, April 12, 2015

KOCHA WA BARCELONA AITUPIA SAFU YAKE YA ULINZI KUFUATIA SARE.

MENEJA wa Barcelona, Luis Enrique amelaumu makosa yaliyofanywa na safu yake ya ulinzi katika kikosi chake ambayo yamewagharimu sare ya mabao 2-2 dhidi ya Sevilla jana. Barcelona walionekana wanaweza kuchukua alama zote tatu katika mchezo huo baada ya Lionel Messi na Neymar kuifungia timu hiyo mabao katika kipindi cha kwanza. Hata hivyo makosa yaliyofanywa na golikipa wa kimataifa wa Chile Claudio Bravo yaliipa ahueni Sevilla baada ya kupata bao kabla ya muda wa mapumziko. Kipindi cha pili Sevilla walitumia vyema makosa ya beki Gerard Pique ambayo yalimpa nafasi Jose Antonio Reyes aliyetoa pande murua lililomaliziwa vyema na Kevin Gamero na kuzifanya timu hizo kugawana alama. Enrique amesema kipindi cha kwanza kikosi cha kilicheza vyema na kupata mabao ya kuongoza lakini pindi Sevilla walivyorudisha bao la kwanza anadhani wachezaji wake walipoteana na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa sare.

No comments:

Post a Comment