MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Raheem Sterling amekumbushwa majukumu yake akiwa kama kioo cha jamii kufuatia picha za hivi karibuni zilizotoka katika gazeti. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 20, alipigwa picha akiwa anavuta shisha. Sterling alikutana na meneja wa Liverpool Brendan Rodgers kwa ajili ya mazungumzo jana na klabu imesisitiza kuwa suala hilo limeshakwisha. Rodgers pia alifanya mazungumzo na winga Jordan Ibe mwenye umri wa miaka 19 ambaye alipigwa picha sambamba na Sterling wakivuta shisha. Tukio hilo limekuja ikiwa imepita wiki moja baada ya mshambuliaji huyo mzaliwa wa Jamaica kukiri kukataa ofa ya mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki kwenye mkataba wake mpya.
No comments:
Post a Comment