CHAMA cha Soka cha Afrika Kusini-SAFA kimetuma salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha ghafla cha mshambuliaji wa zamani wa Bafana Bafana na klabu ya Free State Stars Richard Tebogo Henyekane. Henyekane aliyekuwa na umri wa miaka 31 amefariki dunia leo asubuhi katika ajali ya gari ambalo alikuwa na watu wengine wanne. Kifo chake kinakuja ikiwa imepita miezi minne baada ya kufariki dunia kwa kaka yake Joseph henyekane ambaye pia alikuwa mchezaji wa kulipwa. Rais wa SAFA Danny Jordaan ambaye yuko jijini Cairo, Misri kuhudhuria mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF amesema kifo cha mchezaji huyo kimekuja wakati bado kidonda cha kumpoteza kaka yake hakijapona. Jordaan aliendelea na kudai kuwa SAF inawapa pole familia, marafiki, wachezaji wenzake na mashabiki wake kwa ujumla kwa kuondokewa na mpendwa wao.
No comments:
Post a Comment