MFANYABIASHARA bilionea kutoka Thailand Bee Taechaubol ameafiki makubaliano ya awali ya kununua hisa katika klabu ya AC Milan ya Italia. Bilionea huyo amekuwa katika mzungumzo na rais wa Milan Silvio Belusconi na sasa amefikia makubaliano na kampuni mama inayomiliki klabu hiyo ya Fininvest. Katika taarifa yake Taechaubol amesema ana furaha kubwa kuwa sehemu ya klabu hiyo yenye historia kubwa na kufuatiliwa na watu wengi duniani kote ikiwemo nchi yake. Bilionea aliendelea kudai kuwa kama ukipita katika mitaa ya jiji la Bangkok utashuhudia watu wasiohesabika wakiwa wamevaa fulana za timu hiyo hivyo kuwa sehemu ya klabu ni heshima kubwa kwake. Bado haijawekwa wazi kama ununuzi huo utamfanya Taechaubol kuchukua nafasi ya Berlusconi ambaye amekuwa mmiliki wa klabu hiyo toka Februari mwaka 1986, akiwa mtu aliyeshikilia hisa nyingi kwa kipindi kirefu.
No comments:
Post a Comment