NAHODHA wa Liverpool, Steven Gerrard jana amefunga bao la ushindi katika dakika za majeruhi dhidi ya Queens Park Rangers na kufufua matumaini ya timu hiyo kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Gerrard alifunga bao hilo kwa kichwa katika dakika ya 87 akimalizia mpira wake wa penati aliopiga na kukosa wakati matokeo ya kiwa sare ya bao 1-1. Liverpool ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Philippe Coutinho kabla ya Leroy Fer kusawazisha bao hilo. Wachezaji wa timu zote mbili walivaa vitambaa vyeusi mkononi baada ya taarifa kabla ya mchezo ya kufariki kwa mke wa beki wa QPR Rio Ferdinand aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani matiti. Gerrard pia aliingia na maua na kumpatia kiungo wa QPR Joey Barton aweze kumpa Ferdinand.
No comments:
Post a Comment