Sunday, May 3, 2015

MATTHIAS SAMMER AMKINGIA KIFUA GUARDIOLA.

MKURUGENZI wa michezo wa Bayern Munich, Matthias Sammer amesisitiza Pep Guardiola hayupo katika shinikizo lolote la ndani kufuatia kipigo walichopata dhidi ya Bayer Leverkusen jana. Mabao ya Hakan Calhanoglu na Julian Brandt yaliyofungwa katika kipindi cha pili yaliyosha kuwapa wenyeji Leverkusen ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa wa hao wa Bundesliga katika mchezo uliofanyika Uwanja wa BayArena. Kumekuwa na mjadala katika wiki za karibuni kuhusu uwezo wa Guardiola toka ametua Allianz Arena msimu wa 2014-2015, lakini Sammer amesema kocha huyo na wachezaji wote wanaungwa mkono kwa juhudi zao. Akihojiwa Sammer amesema Guardiola tayari amewaletea mataji matano katika kipindi cha miaka miwili alichokuwa nao hivyo hawapaswi kumlaumu yeye wala wachezaji kwani wamekuwa wakifanya kazi yao vyema. Sammer aliendelea kudai kuwa kikubwa kinachoiathiri timu hiyo msimu huu ni uchovu wa wachezaji wake kutokana na michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika mwaka jana pamoja na majeruhi wengi walionao hivi sasa.

No comments:

Post a Comment