KLABU ya Juventus wametawadhwa mabingwa Serie A kwa mara nne mfululizo baada ya kupambana na kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Sampdoria jana. Katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Luigi Ferraris, Juventus ilikuwa ikihitaji alama moja ili iweze kushinda taji lake la 31 la Serie A lakini walifanikiwa kupata alama zote tatu kupitia baada ya Arturo Vidal kufunga bao pekee katika mchezo huo. Hilo linakuwa taji la kwanza kwa kocha Massimiliano Allegri toka alipokabidhiwa mikoba ya kuinoa Juventus majira ya kiangazi mwaka jana.
Allegri mwenye umri wa miaka 47 alichukua mikoba ya Antonio Conte ambaye alijuzulu wadhifa wake huo siku moja baada ya wachezaji kurejea tayari kwa maandalizi ya msimu. Juventus sasa ina kibarua kingine wakati watakapokwaana na mabingwa watetezi Real Madrid katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne ijayo.
No comments:
Post a Comment