WINGA wa klabu ya Sunderland, Adam Johnson ameachiwa kea dhamana mpaka mwezi ujao baada ya kutokea katika mahakama ya Peterlee. Johnson mwenye umri wa miaka 27 ambaye mwezi uliopita alishakiwa kwa makosa matatu ya kujihusisha katika vitendo vya ngono na msichana mwenye umri chini ya miaka 16, alitokea mahakamani hapo leo. Kesi hiyo imeahirishwa huku Johnson akiachiwa kea dhamana mpaka Juni 3 kesi hiyo itakaposikilizwa tena. Johnson ambaye amewahi kuzitumikia klabu za Manchester City na Middlesbrough, alikamatwa Machi mwaka huu akituhumiwa kujihusisha na ngono na msichana wa miaka 15.
No comments:
Post a Comment