KIUNGO wa kimataifa wa Ghana, Andre Ayew ameteuliwa kuwa mchezaji bora kutoka Afrika anayecheza katika Ligi Kuu ya Ufaransa leo. Ayew amemaliza akiwa kinara akiwazidi Max-Alain Gradel wa Ivory Coast na klabu ya Saint-Etinne na Aymen Abdennour kutoka Tunisia anayekipiga katika timu ya Monaco. Kiungo huyo amekuwa katika kiwango kikubwa msimu huu na kuzivutia klabu mbalimbali nchini Uingereza zikiwemo Liverpool, Tottenham Hotspurs, Arsenal na hata Newcastle United ambao wako katika hatari ya kushuka daraja. Ayew ambaye amekuwa na Marseille kea kipindi cha miaka 10, alitangaza mapema kuwa msimu huu ndio utakuwa wa mwisho kwake kuitumikia timu hiyo.
No comments:
Post a Comment