SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA linatarajia kufanya uchunguzi kuhusiana na kukamatwa kwa kundi la wanahabari nchini Qatar waliokuwa wakiripoti hali ya wafanyakazi wa kigeni kuelekea katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022. Waandishi wanne wa BBC walikamatwa na kuwekwa lupango kwa siku mbili baada ya kufuatiliwa na kudakwa na polisi wakituhumiwa kuingia bila vibali. Katika taarifa yake, FIFA imedai kuwa itaanzisha uchunguzi kuona kama wanahabari hao waliingiliwa uhuru wao wa kutafuta na kutoa habari bila bugdha. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa FIFA inaheshimu uhuru wa habari hivyo hawataweza kufumbia macho suala lolote linaloweza kuhatarisha hilo.
No comments:
Post a Comment