Monday, May 18, 2015

BEKI WA ZAMANI WA PSG AMTAKA DI MARIA KWENDA UFARANSA.

BEKI wa zamani wa Paris Saint-Germain, Alain Roche anadhani winga wa Manchester United Angel Di Maria atakuwa chaguo sahihi katika usajili wa mabingwa hao wa Ufaransa. PSG ilijaribu kumsajili Di Maria msimu uliopita lakini mwenyewe akaamua kutimkia United badala ya Real Madrid. Hata hivyo, nyota huyo wa kimataifa wa Argentina ameshindwa kung’ara Old Trafford hivyo kuhusishwa na tetesi za kuhama majira ya kiangazi. Roche amesema PSG wanapaswa kufanya kila wawezalo kuhakikisha wanamsajili Di Maria kama United wakiamua kumuacha mwishoni mwa msimu huu. Di Maria ana mkataba na United unaomalizika Juni mwaka 2019.

No comments:

Post a Comment