Sunday, May 3, 2015

AMIRI KHAN ATAKA KUPIGANA NA MAYWEATHER.

BONDIA mahiri wa Uingereza Amir Khan amesema meneja wa Floyd Mayweather amemwambia kuwa pambano lao linawezekana baada ya Mmarekani huyo kumtandika Manny Pacquiao jijini Las Vegas leo. Mayweather mwenye umri wa miaka 38 aliendeleza rekodi yake ya kutopigwa katika mapmbano 48 kwa kushinda kwa alama katika pambano dhidi ya Pacquiao. Khan mwenye umri wa miaka 28 ambaye atapambana na bingwa wa zamani wa dunia wa uzani mwepesi wa welter Chris Algieri Mei 30 mwaka huu amesema pia amealikwa kupigana na Pacquiao mwenye umri wa miaka 36. Akihojiwa Khan amesema yuko katika nafasi ya kupambana yeyote kati ya hao wawili lakini yeye anamtaka Mayweather. Khan aliendelea kudai kuwa meneja wa Mayweather, Len Ellerbe alimfuata baada ya pambano hilo na kumwambia kuwa kifedha wanajua litakuwa pambano kubwa hivyo anadhani timu ya Mayweather inahitaji pambano hilo huku timu ya Pacquiao nayo ikihitaji kitu kama hicho. Mayweather amesema baada ya pambano lake kuwa amepanga kustaafu baada ya pambano kupigana pambano moja zaidi Septemba mwaka huu kwasababu hafurahii tena mchezo huo.

No comments:

Post a Comment