KLABU ya Chelsea wamefanikiwa kutawadhwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya kuichapa Crystal Palace kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Stamford Bridge. Bao hilo ambalo lilifungwa Eden Hazard kwa kichwa akimalizia mpira wa penati aliokosa na kuifanya timu hiyo sasa kuivua rasmi ubingwa Manchester City huku kukiwa kumebaki michezo mitatu kabla ya msimu haujamalizika. Hilo linakuwa taji la tatu kwa Jose Mourinho akiwa meneja wa Chelsea na la kwanza katika kipindi chake cha pili cha uongozi. Taji hilo pia linakuwa la tano kwa timu hiyo na yamekuja katika kipindi cha miaka mitano toka miaka kupita miaka 60 toka wanyakuwa taji lao la kwanza.
No comments:
Post a Comment