Wednesday, May 13, 2015

ANCELOTTI AFUNGIWA MECHI ZOTE ZILIZOBAKIA.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti anatarajiwa kuukosa msimu uliobakia wa La Liga baada ya kufungiwa mechi mbili na Shirikisho la Soka la Hispania-RFEF. Adhabu inatokana matamshi ya kkashifu aliyotoa kocha huyo kuwaelekea waamuzi katika mchezo dhidi ya Valencia ambao Madrid walitoa sare ya mabao 2-2 Jumamosi iliyopita. Katika ripoti ya mwamuzi Carlos Clos Gomez aliyechezesha mchezo huo, alidai kuwa Ancelotti alimshambulia kea maneno kuonyesha kutoridhishwa na maamuzi yake mara baada ya mchezo kumalizika. Anncelotti mwenye umri wa miaka 55 sasa atakosa mechi mbili za ligi za Madrid zilizobakia msimu huu, ukiwemo mchezo dhidi ya Espanyol na Getafe.

No comments:

Post a Comment