Wednesday, May 13, 2015

TIKETI ZAPANDA BEI MECHI YA MWISHO YA GERRARD KATIKA UWANJA ANFIELD.

TIKETI kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa Steven Gerrard akiwa nyumbani na Liverpool zimeingia sokoni wiki hii zikiuzwa kea zaidi ya paundi 1,300. Mchezo huo wa Jumamosi hii dhidi ya Crystal Palace utakaofanyika katika Uwanja wa Anfield ndio utakuwa wa mwisho kea nahodha huyo. Kwa kawaida bei ya juu ya tiketi katika jukwaa kuu hufikia kiasi cha paundi 47 lakini safari hii tiketi hizo zimeanzia kuuzwa paundi 100 mpaka 1,300. Gerrard mwenye umri wa miaka 34, atamaliza kipindi chake cha miaka 17 ya kuitumikia Liverpool katika mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Stoke City kabla ya hajahamia katika klabu yake mpya ya Los Angeles Galaxy ya Marekani. Taarifa zinadai kuwa nahodha huyo wa zamani wa Uingereza atatengewa gwaride la heshima kabla ya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment