KIUNGO wa Manchester City, Yaya Toure amekataa kujadili mustakabali wake katika timu hiyo jana wakati alipoulizwa suala hilo katika uzinduzi wa mpango mpya wa vitendo vya kibaguzi wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Toka mwaka jana mustakabali wa Toure umekuwa katika hatihati baada ya wakala wake Dimitri Seluk kuituhumu klabu hiyo kudharau siku yake ya kuzaliwa huku wiki iliyopita akidai kuwa mteja wake ana uwezekano wa kuondoka asilimia 90 katika majira ya kiangazi. Toure ambaye ametimiza miaka 32 leo anahusishwa na tetesi za kwenda katika klabu za Inter Milan na Paris Saint-Germain lakini mwenyewe amekanusha taarifa hizo. Akizungumza na wanahabari, Toure amesema alikuwa na vitu vingi vya msingi vya kujadili na anaona in vya muhimu zaidi ya mustakabali wake katika klabu ya City. Toure mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mara nne, alijiunga na City akitokea Barcelona mwaka 2010 na kuisaidia timu hiyo kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu, moja ya Kombe la Ligi na moja la FA.
No comments:
Post a Comment