BEKI wa klabu ya Everton, Leighton Baines anatarajiwa kukosa michezo mwili ya Ligi Kuu iliyobakia msimu huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu. Baines mwenye umri wa miaka 30 aliumia wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Sunderland uliochezwa Goodison Park. Akihojiwa meneja wa Everton Roberto Martinez amesema Baines amekuwa akisumbuliwa na majeruhi hayo kea kipindi cha miaka mitatu na sasa hategemei nyota huyo kurejea tena uwanjani kabla ya kuanza kea msimu ujao kiangazi. Martinez amesema upasuaji alifanyiwa jana ulikuwa na mafanikio na ana matumaini itatibu tatizo lake hilo ambalo limemsumbua kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment