MSIMU wa soka nchini Hispania umeruhusiwa kumalizika baada ya tishio la kusimamishwa lililotolewa na Shirikisho la Soka la Hispania-RFEF na mgomo wa wachezaji kusogezwa mbele na mahakama ya taifa nchini humo. RFEF walikuwa wakitaka kusimamisha mechi za mwisho wa msimu zilizobakia na umoja wa wachezaji uliamua kuitisha mgomo kutokana na sakata la haki za matangazo. Barcelona wataweza kushinda taji la La Liga Jumapili hii huku wakiwa wamebakia na mchezo mmoja kama wakifanikiwa kuwachapa mabingwa watetezi Atletico Madrid. Fainali ya Kombe la Mfalme ambayo pia itawakutanisha na Barcelona na Athletic Bilbao itaendelea kama ilivyopangwa Mei 30 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment