NAHODHA wa Liverpool, Steven Gerrard ambaye anaondoka mwishoni mwa msimu huu, amesema anajuta kutoshinda taji la Ligi Kuu katika kipindi chote alichoitumikia klabu hiyo. Gerrard mwenye umri wa miaka 34 anatarajiwa kucheza mchezo wake wa mwisho Anfield, Jumamosi hii dhidi ya Crystal Palace kabla ya hajajiunga na Los Angeles Galaxy ya Marekani mwezi ujao. Akihojiwa Gerrard amesema angefurahi zaidi kuondoka Liverpool akiwa na medali ya Ligi Kuu lakini hilo halitawezekana na ndio kitu kikubwa anachojutia kukikosa katika maisha yake ya soka Anfield. Gerrard anaondoka Liverpool akiwa ameichezea mechi zaidi ya 700 katika misimu 17 ambayo amekuwa nao.
No comments:
Post a Comment