Thursday, May 14, 2015

SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LAKANUSHA KUPOKEA FEDHA ZA MSAADA KUTOKA KWA RONALDO.

SHIRIKA la misaada la Save the Children limekanusha taarifa kuwa Cristiano Ronaldo ametoa msaada ya euro milioni saba kea ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Nepal. Kauli ya shirika hilo imekuja kufuatia taarifa kuwa Ronaldo mwenye umri wa miaka 30 ametoa kiasi hicho cha fedha kwenda kusaidia waathirika wa tetemeko hilo. Katika taarifa ya shirika hilo iliyotolewa leo imedai kuwa kuwa Ronaldo akiwa balozi wao amekuwa akipaza sauti kueleza matatizo wanayokutana nayo watoto duniani. Lakini taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa ripoti za hivi karibuni kuwa Ronaldo ametoa fedha kwa shirika hilo la Save the Children kea ajili ya waathirika wa Nepal sio za kweli. Zaidi wa watu 8,000 walifariki dunia kea tetemeko kubwa lililoikumba nchi hiyo Aprili 25 mwaka huu kabla ya lingine kutokea Mei 12 na kuuwa wengine 16.

No comments:

Post a Comment