Friday, May 15, 2015

FAINALI EUROPA LEAGUE KUZIKUTANISHA SEVILLA NA DNIPRO.

KLABU ya Dnipro itakwaana na mabingwa watetezi Sevilla katika fainali ya michuano ya Europa League baada ya kuitandika Napoli ya Italia jana kwa bao 1-0. Bao pekee katika mchezo huo lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Ukraine Yevhen Seleznyov lilitosha kuing'oa Napoli kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1 katika michezo miwili waliyokutana. Sevilla wao walijihakikishia nafasi ya kutetea taji lao kwa kuichapa Fiorentina kwa mabao 2-0 na kuwafanya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-0. Fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa jijini Warsaw, Poland Mei 27 mwaka huu na mshindi atafunzu moja kwa moja michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani.


No comments:

Post a Comment