WACHEZAJI wanne wa klabu ya River Plate wamekimbizwa hospitali baada ya kupuliziwa pilipili na mashabiki wa Boca Juniors hatua ilipelekea mchezo wao wa Copa Libertadores kuahirishwa. Mchezo huo wa maruadiano hatua ya mtoano uliofanyika Buenos Aires, Argentina, ulisimamishwa wakati timu hizo zikiwa hazijafunga baada ya wachezaji kushambuliwa wakati wakitoka katika vyumba vyao wakati wa mapumziko. Tukio hilo limelaaniwa vikali napande zote mbili huku rais wa Boca Juniors Daniel Angelici akidai kuwa watafanya kila wawezalo kushirikiana na polisi ili kuwanasa wahalifu hao. Picha za video zilizkuwa zikiwaonyesha wachezaji wa River Plate Leonardo Ponzio na Leonel Vangioni wakisugua macho yao huku wachezaji wengine wakinawa maji usoni baada ya kupuliziwa pilipili. Baadhi ya wachezaji walisikika wakilalama kuwa hawaoni huku macho yao yakiwaka moto hatua ilipelekea mwamuzi kusitisha pambano hilo.
No comments:
Post a Comment