Tuesday, May 5, 2015

BLATTER HAJUI ANACHOKIFANYA - MARADONA.

NGULI wa soka wa Argentina, Diego Maradona amerusha makombora kwa Sepp Blatter akidai kuwa rais huyo wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ameigeuza ofisi hiyo kama isiyokuwa na uongozi. Maradona mwenye umri wa miaka 54 anamuunga mkono Prince Ali bin Al-Hussein katika uchaguzi wa urais wa FIFA unaotarajiwa kufanyika Mei 29 na Maradona ambaye amewahi kushinda Kombe la Dunia mwaka 1986 akiwa na Argentina amesisitiza kuwa muda wa mabadiliko umefika. Akihojiwa Maradona amesema kama asingeamini kuwa Prince Ali ataweza kuja kuwa rais mzuri asingekuwepo hapo. Maradona aliendelea kudai kuwa ulimwengu wa soka unafahamu ndani ya FIFA hakuna uongozi kwani ni mtu mmoja pekee ambaye anaamua kila kitu lakini hajui lolote hivyo ni wakati wa kufanya mabadiliko. Nguli huyo amesema watu wake wanapaswa kumshauri aondoke kwani amekuwa akileta matatizo katika soka toka aingie madarakani.

No comments:

Post a Comment