NGULI wa zamani soka Javier Zanetti amesema hatasahau siku hiyo ambayo klabu ya Inter Milan ilipoamua kusimamisha matumizi ya fulana yenye namba nne kwa heshima yake jana. Beki huyo wa kimataifa wa Argentina alitundika daruga zake rasmi mwishoni mwa msimu uliopita akiwa ameisaidia klabu hiyo kushinda mataji matano ya Serie A, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya, moja la Klabu Bingwa ya Dunia na manne ya Kombe la Dunia katika kipindi cha maika 19 aliyoitumikia. Klabu hiyo ilitangaza kuipumzisha jezi namba nne kwa heshima yake na walitimiza adhma hiyo jana katika mchezo wa hisani uliochezwa katika Uwanja wa San Siro. Zanetti aliwashukuru marafiki zake wote waliokuwepo katika mchezo huo na kudai kuwa kamwe hawezi kuisahau siku hiyo huku pia akiwashukuru watu wote waliohudhuria mchezo huo wa hisani. Mkongwe huyo aliendelea kudai kuwa pamoja na kuwa amestaafu soka lakini upendo wake na mashabiki wa klabu hiyo utabakia milele na uhusiano wao kamwe hautakwisha.
No comments:
Post a Comment