OFISA mkuu wa zamani wa Liverpool, Rick Parry anaamini mpango uliokuwa ukisubiriwa kipindi kirefu wa upanuzi wa Uwanja wa Anfield ni hatua kubwa kwa timu hiyo kuelekea kulingana na mahasimu wao wengine wa Ligi Kuu. Kazi ya upanuzi tayari imeanza ambapo itakuja kushuhudia uwanja ukiongeza uwezo wa kuingiza mashabiki kutoka 45,500 mpaka 54,000 ifikapo msimu wa 2016-2017 baada ya hatimaye kuruka vikwazo kadhaa vilivyokuwa vikiwazuia kufanya hivyo. Akihojiwa Parry amesema upanuzi huo ni hatua kubwa kuelekea katika njia sahihi. Parry aliendelea kudai kuwa ni jambo muhimu kuwa na sheria ya kudhibiti matumizi ya fedha katika Ligi Kuu pamoja na Ulaya kwasababu inazibana klabu kujiendesha kutokana na jinsi wanavyoingiza mapato yao hivyo kwa Liverpool mapato lazima yataongezeka. Parry amesema amekuwa akilishughulikia suala hilo kwa kipindi cha miaka 10 lakini haikuwa kazi rahisi kulikamilisha katika uongozi wake hivyo anafurahi kuona hatimaye linafanyika.
No comments:
Post a Comment