MAOFISA wanne wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF wako nchini Rwanda kukagua maendeleo ya maandalizi ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani itakayofanyika nchini humo kuanzia Januari 16 na kumalizika Februari 7 mwakani. Wajumbe hao wa CAF ambao ni Mkurugenzi wa Michezo Shereen Arafa, Mkurugenzi wa IT Tarek El Deeb, Mkurugenzi wa Habari Solomon Binyam na Ofisa Masoko Oman Said, kwa pamoja na wanatarajiwa kukagua vitu mbalimbali mojawapo vikiwa viwanja vinne vitakavyotumika, viwanja vya mazoezi, hoteli, usalama na masuala ya usafiri. Viwanja watakavyotembelea ambavyo ndio vitatumika katika michuano hiyo in pamoja na Uwanja wa Amahoro na Uwanja wa Manispaa wa Kigali vyote vikiwa jijini Kigali, Uwanja wa Huye uliopo kusini na Uwanja wa Umuganda uliopo Rubavu. Pia watatembelea kukagua viwanja vya mazoezi, hoteli ambazo timu na maofisa wengine wa shirikisho hilo watakazofikia pamoja na suala zima la usafiri. Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni Libya ambao waliichapa Ghana katika mchezo wa fainali uliofanyika jijini Cape Town, Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment