Sunday, May 10, 2015

GUARDIOLA KUTIMKIA CITY.

MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani, Dietmar Hamann amedai Pep Guardiola anatarajia kuondoka Bayern Munich kuelekea Manchester City katika majira ya kiangazi. Kumekuwa na taarifa zilizosambaa jana kuwa kocha huyo wa zamani wa Barcelona amefikia makubaliano ya awali juu ya kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini katika msimu wa 2015-2016. Guardiola amefanikiwa kutetea taji la Bundesliga msimu huu, lakini kocha huyo amejikuta katika kipindi kigumu zaidi katika miaka miwili aliyoinoa Bayern baada ya kupoteza mchezo wake nne mfululizo jana. Akihojiwa Hamman ambaye amewahi kuichezea Bayern amesema alitumiwa meseji na mtu wa karibu aliyedai kuwa City walifanya mazungumzo na Guardiola miezi miwili iliyopita na akawakatalia lakini kuna mazungumzo mapya yaliyoanza. Hamman aliendelea kudai kuwa katika mazungumzo mapya kuna dalili za makubaliano hivyo Guardiola anaweza kwenda City msimu ujao.

No comments:

Post a Comment