MCHEZAJI soka wa ligi ndogo, Tim Nicot amekuwa mchezaji wa pili wa Ubelgiji kufariki kwa mshtuko wa moyo katika kipindi cha wiki mbili zilizopita. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anayecheza timu ya daraja la nne ya Wilrijk-Beerschot alikuwa akicheza katika mashindano huko Hemiksen wakati alipoangka Ijumaa iliyopita. Nicot aliwekwa katika hali ya kutojitambua hospitalini huku akisaidiwa kupumua na mashine kabla ya klabu yake kuthibitisha kifo chake leo. Mwishoni mwa mwezi uliopita beki wa klabu ya Lokeren ya Ubelgiji Gregory Mertens mwenye umri wa miaka 24 alifariki baada ya kuanguka wakati akicheza mechi ya wachezaji wa akiba. Miaka mitatu iliyopita kiungo wa Bolton Wanderers Fabrice Muamba akiwa na umri wa miaka 23 kipindi hicho alipata mshtuko wa moyo katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Tottenham Hotspurs lakini alifanikiwa kuzinduka baada ya kushindw akupumua kwa dakika 78.
No comments:
Post a Comment