MENEJA wa klabu ya Real Sociedad David Moyes amezipasha klabu za Ligi Kuu zinazomuwinda kuwa hana mpango wa kwenda popote kufuatia tetesi kuwa atarejea nchini Uingereza. Kocha huyo raia wa Scotland alitimuliwa na Manchester United baada ya kuinoa katika kipindi cha miezi 10, Novemba mwaka jana kutokana na klabu hiyo kutofurahishwa na matokeo. Moyes alirejea tena uwanjani akiwa kocha wa Sociedad mazingira ambayo alikuwa hana mazoea nayo katika Ligi Kuu ya Hispania. Wiki za karibuni kumezuka tetesi kuwa klabu za West Ham United na Newcastle United zimekuwa zikitaka saini yake lakini mwenyewe amedai hana mpango wa kuondoka Hispania kwasasa. Akihojiwa Moyes amesema kwasasa anataka kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao jambo ambalo amefikia hatua nzuri hivyo hawezi kuacha mpaka atomize adhma yake hiyo.
No comments:
Post a Comment