Thursday, May 7, 2015

PACQUIAO AFANYIWA UPASUAJI WA BEGA.

BONDIA Manny Pacquiao amefanyiwa upasuaji wa bega alilolalamikia kuchangia kupigwa katika pambano lake na Floyd Mayweather jijini Las Vegas. Bondia huyo raia wa Ufilipino ameshitakiwa na mamlaka ya Nevada baada ya kutuhumiwa kudanganya kuhusu afya yake wakati alipofanyiwa vipimo kabla ya pambano. Daktari aliyemfanyia upasuaji huo Neal ElAttrache alithibitisha taarifa hizo na kudai kuwa bondia huyo mwenye umri wa miaka 36 anaendelea vyema lakini anaweza kukaa nje ya ulingo kea kipindi cha mwaka mmoja. Pacquiao alikataliwa kupigwa sindano ya kuzuia maumivu saa mbili kabla ya pambano kwasababu Tume ya Wanamichezo ya Nevada-NAC ilikuwa haijajulishwa kuhusu majeruhi yake kabla. Mayweather mwenye umri wa miaka 38 alikaririwa na luninga ya michezo ya ESPN akidai kuwa yuko tayari kurudiana na Pacquiao katika kipindi cha miezi 12, ingawa Mmarekani huyo mara kadhaa amesisitiza kuwa anataka pambano moja la mwisho huku Mwingereza Amir Khan akipewa nafasi kubwa.

No comments:

Post a Comment