SHIRIKISHO la soka la Ulaya-UEFA linajiandaa kulegeza sheria ya mwaka 2011 inayozuia vilabu vya bara hilo kufanya matumizi ya ziada. Katika mahojiano na redio ya Ufaransa RTL, rais wa UEFA Michel Platini amesema kuwa sheria hiyo ilikuwa ikifanya kazi vizuri lakini itaboreshwa zaidi mwishoni mwa msimu huu. Hatua hiyo inafuatia ripoti katika gazeti la Le Parisien siku ya jumapili iliyosema kuwa kuna mabadiliko muhimu yatakayofanywa katika sheria hiyo. Manchester City, Barcelona na Paris Saint-Germain wamekuwa wahanga wa kwanza wa sheria hiyo baada ya kupigwa faini na adhabu mwaka jana.
No comments:
Post a Comment