Tuesday, May 5, 2015

URAIS FIFA 2015: AL HUSSEIN ADAI YUKO RADHI KUMUUNGA MKONO MGOMBEA MMOJA ATAKAYELETA MABADILIKO.

PRINCE Ali Bin Al-Hussein anaweza kufikiria kujitoa katika kinyang’anyiro cha urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ili kuruhusu mgombea mmoja kushindana na Sepp Blatter. Al-Hussein kwasasa anasimama katika kinyang’anyioro hicho dhidi ya Blatter, Michael van Praag wa Uholanzi na nyota wa zamani wa kimataifa wa Ureno Luis Figo. Akihojiwa Al Hussein ambaye anatokea Jordan amesema jambo la muhimu ni kumuunga mkono mgombea ambaye wanajua ana nafasi nzuri ya kuleta mabadiliko katika FIFA. Al Hussein aliendelea kudai kuwa kuna hatua wanaweza kufikia na kujadili suala hilo. Blatter mwenye umri wa miaka 78 anagombea kipindi kingine cha tano huku wajumbe 209 wa FIFA wakitarajiwa kupiga kura katika uchaguzi utakaofanyika Mei 29 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment