Monday, June 22, 2015

CITY YAONGEZA OFA NYINGINE KWA STERLING.

KLABU ya Manchester City imeripotiwa kuwa inajiandaa kutuma ofa ya mwisho ya paundi milioni 45 kwa ajili ya mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling. Ofa mbili za City za paundi milioni 30 na paundi milioni 35 tayari zimeshakataliwa lakini sas wanaamini ofa hiyo mpya inaweza kukamilisha dili hilo. Kwa upande wa Sterling tayari ameshweka bayana kuwa anataka kuondoka Liverpool ingawa bado hajawasilisha ombi rasmi la kuondoka kwa uongozi wa klabu hiyo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 anaweza kufanya hivyo ili kuishinikiza Liverpool kwani kadri siku zinavyokwenda Sterling anaonekana hataki tena kuendelea kuwepo Anfield. Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers anaweza kuridhika kumuuza Sterling kwa paundi milioni 45 kwani zitamuwezesha kukamilisha mipango yake ya kuwawinda Nathaniel Clyne na Christian Benteke.

No comments:

Post a Comment