MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Mario Mandzukic anakaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda klabu ya Juventus kea ada inayokadiriwa kufikia euro milioni 18. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 alitua jijini Turin jana na kufanyiwa vipimo vya afya mapema asubuhi ya leo. Juventus wanataraji kutoa euro milioni 15 kwa ajili ya Mandzukic huku zingine euro milioni tatu wakitarajiwa kulipa kidogo kidogo. Nyota huyo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu ambao utamuwezesha kulipwa kitita cha paundi milioni 3.5 kwa mwaka huku kukiwa na uwezekano wa kuongezwa mwaka mmoja zaidi. Mandzukic raia wa Croatia ameitumikia Atletico kwa msimu mmoja pekee toka alipotua akitokea Bayern Munich majira ya kiangazi mwaka jana.
No comments:
Post a Comment