Friday, July 3, 2015

ANELKA KUWA KOCHA MCHEZAJI MUMBAI CITY FC.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Chelsea Nicolas Anelka anatarajiwa kurejea katika timu ya Mumbai City FC akiwa kama kocha mchezaji kwa msimu wa pili wa Ligi Kuu ya India maarufu kam Indian Super League. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36, ambaye aliifungia Mumbai mabao mawili katika msimu wa kwanza wa ligi hiyo yenye timu nane mwaka jana, pia amewahi kucheza na kufundisha katika timu ya Shanghai Shenhua ya China mwaka 2012. Akihojiwa, Anelka aliushukuru uongozi wa klabu hiyo kwa kumpa nafasi ya kuinoa lakini na wakati huohuo yeye mwenyewe akiwa mchezaji. Klabu hiyo ambayo inamilikiwa na nyota wa filamu huko Bollywood Ranbir Kapoor, ilimaliza katika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment