MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Nigeria, Peter Odemwingie amesaini nyongeza ya mwaka mmoja katika mkataba wake na klabu ya Stoke City. Winga huyo mwenye umri wa miaka 33 sasa anatarajiwa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Ligi Kuu mpaka majira ya kiangazi mwakani huku kukiwa na kipengele cha kuongezwa miezi mingine 12. Akihojiwa Odemwingie amesema anafurahia kuendelea kubakia Stoke na kuwashukuru wale wote ambao wamekuwa wakiimunga mkono kwa wakati wote. Msimu uliopita ulikuwa wa majanga kwa Odemwingie baada ya kupata majeruhi mabaya yaliyomuweka nje kwa kipindi cha miezi nane kabla ya kurejea tena uwanjani zikiwa zimebaki mechi tano msimu kumalizika. Nyota huyo alitua Stoke akitokea Cardiff City Januari mwaka 2014 ambapo toka wakati huo amecheza mechi 23 na kufunga mabao matano.
No comments:
Post a Comment