Friday, July 3, 2015

JUVENTUS YAMKOMALIA VIDAL.

OFISA mkuu wa Juventus, Giuseppe Marotta amesema klabu hiyo haijapata ofa yeyote kwa ajili ya Fernando Llorente na Arturo Vidal ambao wanawindwa na Real Madrid. Llorente alilazimika kucheza sehemu kidogo ya msimu akiwa na Juventus msimu uliopita baada ya mshambuliaji wa zamani wa Madrid Alvaro Morata kumpora nafasi yake wakati Vidal yeye amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwindwa na timu hiyo kwa misimu ya hivi karibuni. Meneja mpya wa Madrid, Rafa Benitez ameripotiwa kutaka kuwasajili wawili hao lakini wakati Llorente akiwa na uwezo wa kuhama kiangazi hiki, Marotta amesema klabu haina mpango wowote wa kumruhusu Vidal kuondoka. Marotta aliendelea kudai kuwa hakuna ofa yeyote iliyotoka kwa ajili ya wawili hao lakini kwenye mipango yao wameamua kutomuachia Vidal kwa wakati huu.

No comments:

Post a Comment