Saturday, July 18, 2015

ARSENAL INAHITAJI KUSAJILI WANNE ZAIDI ILI WAWEZE KUIFIKIA CHELSEA - HENRY.

NGULI wa zamani wa soka wa Ufaransa, Thierry Henry amesema Arsenal inahitaji kusajili wachezaji wengine wanne zaidi kama wanataka kuchuana na Chelsea katika kugombea taji la Ligi Kuu. Arsenal walimaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita, wakiwa nyuma ya Chelsea ambao ndio waliokuwa mabingwa, kwa alama 12. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger tayari ameshafanya usajili wake wa kwanza katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi kwa kumchukua Petr Cechkutoka Chelsea lakini Henry amesema wachezaji zaidi wanahitaji ili waweze kushindania taji. Akihojiwa Henry amesema anafikiri kikosi cha sasa cha Arsenal kina ari, wachezaji wa kiwangi cha juu na morali ya ushindi lakini bado wanahitaji wachezaji kama wanne zaidi ili waweze kuikaribia Chelsea.

No comments:

Post a Comment