Saturday, July 18, 2015

KAKA NDIYE MCHEZAJI ANAYELIPWA ZAIDI MAREKANI.

KIUNGO wa kimataifa wa Brazil, Kaka ndiye mchezaji anayelipwa zaidi katika Ligi Kuu ya Marekani-MLS akikunja kitita cha dola milioni 7.167 kutoka klabu ya Orlando City. Nyota huyo wa zamani wa AC Milan na Real Madrid amemzidi mshambuliaji wa zamani wa Juventus anayecheza Toronto, Sebastien Giovinco anayepata kitita cha dola milioni 7.115. Wachezaji nyota wa Uingereza Frank Lampard na Steven Gerrard nao hawako mbali kwani wako nafasi ya tatu na nne wakikunja kitita cha dola milioni 6.332 kwa Gerrard katika klabu ya Los Angeles Galaxy na dola milioni sita kwa Lampard akiwa New York City FC. Wengine na Andrea Pirlo anayelipwa dola milioni 2.315 na David Villa wote wakiwa katika klabu ya New York City huku Robbie Keane naye akikunja dola milioni 4.5 kutoka Galaxy.

No comments:

Post a Comment