KLABU ya Atletico Madrid imekubali kumsajili mshambuliaji wa FC Porto Jackson Martinez kwa kitita cha paundi milioni 24.8. Martinez alikuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Arsenal lakini Porto walithibitisha kukubali kitita hicho cha fedha kutoka kwa Atletico. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 alihamia Porto mwaka 2012 na kufanikiwa kufunga mabao 67 katika mechi 90 alizocheza huku akimaliza kama kinara wa mabao katika Ligi Kuu ya Ureno kwa msimu yote mitatu ambayo amekuwa huko. Martinez ambaye anachukua nafasi ya Mario Mandzukic aliyejiunga na Juventus, amesema anafuraha kubwa kutokana na uhamisho huo. Mandzukic amekwenda Juventus kuziba nafasi ya mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Carlos Tevez ambaye amerejea nyumbani katika klabu yake ya Boca Juniors.
No comments:
Post a Comment