Wednesday, July 1, 2015

BARCELONA YAIFUATA RASMI JUVENTUS KWA AJILI YA POGBA.

Klabu ya Barcelona wanajipanga kuweka wazi rasmi nia yao ya kutaka kumsajili Paul Pogba wakati wakurugenzi Ariedo Braida na Alberto Soler kusafiri leo kueekea nchini Italia kukutana na rais wa Juventus Giuseppe Marotta. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa mchezaji anayewindwa na klabu nyingi katika kipindi hiki cha usajili wa kiangazi huku Real Madrid, Paris Saint-Germain, Chelsea na Manchester City pia zikionyesha nia ya kuwinda saini yake. Pogba amekuwa katika mipango ya usajili ya Barcelona pamoja na klabu hiyo kufungiwa kusajili mchezaji yeyote mpaka Januari mwakani. Huku uchaguzi wa rais wa klabu hiyo ukiwa umebaki wiki mbili, wagombea wote akiwemo rais wa sasa Josep Maria Bartomeu na rais wa zamani Joan Laporta wote wamejinadi kutaka kumsajili kiungo huyo.

No comments:

Post a Comment