Wednesday, July 1, 2015

MAZEMBE YATHIBITISHA LILLE KUTAKA KUMSAJILI KALABA.

KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC imethibitisha kuwa wamepokea maombi rasmi kutoka klabu ya Lille ya Ufaransa ya kutaka kumsajili nahodha wa kimataifa wa Zambia Rainford Kalaba. Rais wa Mazembe Moise Katumbi amesema mabingwa hao wa DRC kwasasa wanaijadili ofa ambayo imetolewa na Lille. Kalaba amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Lille kufuatia kocha wa zamani wa Zambia Herve Renard kuteuliwa kuinoa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa Mei mwaka huu. Akihojiwa Katumbi alithibitisha taarifa huku akidai kuwa mazungumzo kati ya klabu hizo mbili yanaendelea kwani wanataka kuhakikisha mustakabali wa Kalaba unakuwa mzuri. Kalaba amekuwa akiitumikia Mazembe toka mwaka 2010 kufuatia kuchukuliwa kwa mkopo na klabu hiyo yenye maskani yake Lubumbashi akitokea timu Sporting Braga ya Ureno kabla ya kununuliwa moja kwa moja msimu uliofuata.

No comments:

Post a Comment