MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Thomas Muller amesisitiza anataka kuendelea kubakia Bayern Munich na kupuuza taarifa kuwa anaweza kuhamia Manchester United katika kipindi hiki cha kiangazi. Sambamba na mchezaji mwenzake wa Bayern, Bastian Schweinsteiger, Muller amekuwa akitajwa katika tetesi kuwa anaweza kwenda Old Trafford kuungana na kocha wake wa zamni Louis van Gaal. Akihojiwa kuhusiana na hilo Muller amesema ni heshima kubwa kwake kusikia kuwa anawindwa na klabu nyingine kubwa kwani hiyo inamaanisha juhudi zake anazofanya zinazaa matunda. Hata hivyo nyota huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa anafurahia kuendelea kuitumikia Bayern mpaka hapo mkataba wake utakapomalizika mwaka 2019.
No comments:
Post a Comment