KLABU ya Shakhtar Donetsk imethibitisha kukubali kupokea kitita cha euro milioni 30 kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji wao Douglas Costa kwenda Bayern Munich. Klabu hiyo ya Ukraine ilibanisha kufikia makubaliano na mabingwa hao wa Bundesliga leo na kumshukuru nyota huyo wa kimataifa wa Brazil kwa kipindi cha miaka mitano ambacho wamekuwa naye. Shakhtar walithibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wao na kumtakiwa kila la heri Costa katika maisha na changamoto mpya anayokwenda kukutana nayohuko Ujerumni. Costa mwenye umri wa miaka 24 atakuwa winga wa ziada katika kikosi cha Bayern kilicho chini ya Pep Guardiola ambacho msimu uliopita kilisuasua kupata mbadala kutkana na Arjen Robben na Franck Ribery kuumia.
No comments:
Post a Comment